Pages

July 12, 2008

AMANDA, MPENI KURA KESHO NDO KESHO

Shindano la 57 la kumtafuta Miss Universe 2008 linatarajiwa kufikia tamati Jumapili hii tarehe 13 Julai huko Nha Trang,Khanh Hoa nchini Vietnam katika ukumbi wa Crown Convention Centre. Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo, shindano hilo litaonyesha moja kwa moja au ‘live” katika vituo mbalimbali vya televisheni ulimwenguni huku nchini Tanzania kituo cha TBC 1 kikifanya hivyo pia. Majaji wa fainali hizo wametajwa kuwa ni Donald Trump Jr(mtoto wa bilionea Donald Trump ambaye pia ndio bosi mkuu wa Miss Universe), Mwanamitindo na mjasiriamali maarufu Roberto Cavalli,muigizaji na mrembo Nadine Velazquez(anaonekana katika show maarufu ya kituo cha televisheni cha NBC iitwayo My Name is Earl), TV Presenter na mshindi wa Miss Universe 2004 Jennifer Hawkins, mtia nakshi maarufu Louis Licari na mpambaji maarufu John Nguyen.Majaji hao watafanya kazi yao katika mavazi ya kuogelea(swimsuit), mavazi ya jioni(evening gowns) na pia ujibuji wa maswali. MCs wa onyesho hilo watakuwa Jerry Springer na Mel B(kutoka kundi maarufu la zamani,Spice Girls).Burudani inatarajiwa kutolewa na Lady GaGa anayetamba na wimbo wake Just Dance.
Posted by Picasa

No comments:

Post a Comment