Pages
▼
June 18, 2008
Karibu Bongo Kelly Rowland
Bila shaka utakuwa bado unalikumbuka kundi maarufu la muziki lililokuwa linajulikana kama Destiny’s Child kutoka nchini Marekani. Miongoni mwa mabinti waliokuwa wanaunda kundi hilo ni Kelly Rowland(pichani).Wenzake walikuwa ni Beyonce Knowles(mke wa Jay Z hivi sasa) na Michelle Williams. Kundi hilo lilivunjika rasmi mwaka 2005 ingawa mara moja moja bado huwa inatokea wakafanya maonyesho pamoja.
Baada ya kuvunjika kwa kundi lao na kila mmoja kuendelea kivyake na shughuli za kimuziki,uigizaji nk, Kelly Rowland amekuwa akijitolea sana kwa huduma za kijamii.Hali hiyo ndio imemfanya achaguliwe hivi karibuni kuwa Balozi wa Taasisi ya MTV Staying Alive ambayo imejikita katika kupigana vita na maradhi ya ukimwi pamoja na matokeo yake kama vile kuwanyanyapaa walioathirika nk.
Ni katika wadhifa huo wa “ubalozi” ambapo Kelly Rowland anatarajiwa kutua nchini Tanzania hivi leo ikiwa ni katika ziara yake katika nchi kadhaa za Afrika ikiwa na nia ya kueneza ujumbe na kuendeleza kazi za taasisi hiyo.
Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania ambao ndio wenyeji wake,Kelly Rowland anatarajia kutembelea vituo kadhaa vinavyojishughulisha na mapambano dhidi ya ukimwi na pia kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake. Akimaliza ziara yake nchini Tanzania,Kelly Rowland anatarajiwa kuelekea Kenya na kisha Ghana,Msumbiji na Angola.
Halafu bonyeza hapa uone jinsi mwanamuziki huyu na nduguze walivyopewa heka heka na nyani katika mojawapo ya nchi za kiafrika anazozitembelea.
By BC.
No comments:
Post a Comment